January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kondo Bungo: Lindeni kura zenu

Spread the love

MGOMBEA ubunge wa Mbagala kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Kondo Bungo ametaka wapigakura wa jimbo hilo wasibabaishwe na amri haramu za mawakala wa CCM, badala yake wabakie karibu na vituo wakishapiga kura kulinda kura zao zisifanyiwe ufisadi. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Katika mkutano wake wa kampeni jana eneo la Moringe, Kata ya Mbagala, amesema wananchi wasikubali kurubuniwa na kwa rushwa ambayo CCM wanapita nyumba kwa nyumba wakihonga pesa ili wachaguliwe.

Bungo ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuzingatia haki ya wananchi ya kuchagua kiongozi wamtakaye kwa uchaguzi ulio huru na wa haki ili kuitunza amani.

“Tunaiasa Tume kuzingatia haki katika uchaguzi huu kulingana na matukio ya historia mbaya ya kukandamiza haki ya wananchi,’’ amesema Bungo anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Pia amesema atafunga kampeni yake ya kuomba kura za kuwakilisha jimbo kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano, kwa mkutano viwanjani Mbagala Zakheim, jijini Dar es Salaam. Jioni alihutubia wakazi wa Kata ya Charambe, viwanja vya Maliasili.

error: Content is protected !!