October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kombora la Msigwa, Polepole ajitetea

Humphrey Polepole, Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Spread the love

MANENO ya Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini baada ya kutoka jela, yamemtumbukia nyongo Humphrey Polepole ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaandika Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Katika ujumbe wake kupitia ukuraza wa twitter, ameeleza kusikitishwa na kauli ya Msigwa huku akimtaka kuwa na shukrani.

“Alikuwa jela, ndugu wakalipa faini mie nikatumwa kumtoa. Sijaelewa hoja ya kununuliwa inatoka wapi? Naona uko suggestive, huko sipo.

“True (kweli), Nchi ni kubwa kuliko familia yako, ila ni familia walichanga 2m (milioni mbili) na Mkweo (Rais John Magufuli) kwa huruma akamalizia 38m, Imeandikwa “iweni watu wenye shukrani.” Ameandika Polepole.

Msigwa akielezea mkasa wa kutolewa kwake na jela tarehe 12 Machi 2020, alisema alishangaa kumuona Polepole akisimamia jambo ambalo lingefanywa na familia yake.

Alitoa kauli hiyo mbele ya waandishi wa habari juzi tarehe 13 Machi 2020. Ni baada ya kuelezwa Polepole alitaka kutumia nafasi ile kwa maslahi ya kisiasa.

“Mimi natoka nje, … kuna kamera wakati juzi wakina Halima (Halima Mdee) wanatoka, kamera hazipo, zimetoka wapi? Natoka nje wanataka kunipiga picha, nikasema nirudishweni gerezani.

“Nataka nimueleze Polepole, i can’t be reduced to that level (siwezi kushushwa (hadhi) kwa kiwango hicho). Mimi ni mtu ninaejitambua, i know what I’m doing (najua ninachokifanya),… Siwezi kununuliwa kwa vipande thelathini vya fedha.

Msigwa alisema, Polepole si mwanafamilia yao na Gerson Msigwa, msemaji wa Ikulu pia sio sehemu ya familia yao, na kwamba mambo ya kifamilia humalizwa na wanafamilia.  

error: Content is protected !!