November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kombe la Mapinduzi kuanza Januari Mosi

Spread the love

MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi inatarajia kuanza kuchezwa Januari Mosi, 2019 na kumalizika Januari 13, visiwani Zanzibar ambayo itahusisha timu tisa ambazo zitawekwa kwenye makundi mawili huku kundi A litakuwa na timu nne na kundi B timu tano. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kundi A litakuwa na timu za Chipukizi, Mlandege, KMKM na Simba, huku kundi B likihusisha bingwa mtetezi wa michuano hiyo katika mwaka uliopita klabu ya Azam FC, Malindi, Yanga, Jamhuri na KVS.

Azam wanatarajia kushuka dimbani Januari 2 kuvaana na Jamhuri, huku Yanga watatupa karata yao ya kwanza Januari 3 watakapowavaa KVS, kwa upande wa Simba watacheza dhidi ya Chipukizi januari 4.

Taarifa kutoka kwa kamati ya maandalizi ya michuano hiyo imeeleza kuwa mshindi wa kwanza wa michuano hiyo atazawadia kiasi cha Sh. 15 milioni, medali za dhahabu pamoja na kombe.

error: Content is protected !!