January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kombani: Ombeni vibali vya kuvuna miti

Spread the love

SERIKALI imezitaka halmashauri kuomba vibali maalum vya uvunaji miti kwa ajili ya matumizi ya utengenezaji wa madawati. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa bungeni leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Selina Kombani alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya (CCM).

Bulaya alitaka kujua ni kwanini halmashauri nyingi zinashindwa kuvuna misitu kwa ajili ya utengenezaji wa madawati wakati wapo wanafunzi wengi wanakaa chini.

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Mufindi Kusini, Menrad Kigola (CCM) alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuwatafutia maeneo mbadala wananchi wa vijiji vya Swala, Kihanga, Mkonge na maeneo mengine ambayo yalichukuliwa na kampuni ya MPM, Unilever tea na idara ya misitu kwa ajili ya kilimo cha chai na upandaji wa miti.

Kigola alisema kutokana na wananchi hao kukosa maeneo wanajikuta wakikosa maeneo ya kilimo, ufugaji na ujenzi wa nyumba za kudumu.

Akijibu maswali hayo, Kombani amesema halmashauri zinatakiwa kuomba vibali maalum kwa ajili ya uvunaji wa miti na kutengeneza madawati.

Katika maelezo yake, Kombani amesema wakati mwingine vibali vinashindikana kutolewa kutokana na waombaji kugeuza matumizi yaliyokusudiwa na kujikuta wanatumia vibali hivyo kwa matumizi yasiyo halali.

Amesema kuwa maeneo ambayo yalichukuliwa na kiwanda cha karatasi kati ya mwaka 1978 na 1982, yalikuwa wazi nje ya makazi ya wanavijiji na hayakuwa yanatumiwa na mtu yoyote.

error: Content is protected !!