July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Komba asimangwa mitandaoni, familia yalalamika

Mtoto wa marehemu, John Komba, Gerald Komba (mwenye shati jeupe)

Spread the love

MTOTO wa aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM), John Komba, amelalamikia baadhi ya wananchi wanaosambaza kashfa za baba yake. Anaripoti Sarafina Lindwino…(endelea).

Gerald Komba, mtoto wa tatu wa hayati John Damian Komba amesema, mitandao karibu yote ya kijamii kumejaa “nukuu chafu za baba yake.” Nukuu hizo, ni zile mbazo alizitoa wakati wa uhai wake.

“Ninawaomba Watanzania wenzagu kuacha kusambaza maneno ya kashfa kwenye mitandao, haswa baada ya mhusika kufariki dunia,” ameeleza Gerald.

Kile anachoita Gerald nukuu chafu, ni ila hadi kufikia leo huko kwenye mitandao ya kijamii kumejaa nukuu zake  chafu ambazo alikuwa akizitoa enzi za uhai wake.

Gerald ameeleza jinsi anavyoumizwa na maneno ya mitandaoni kuhusiana na kifo cha baba yake.

Ametaja moja ya nukuu ambayo imeshika kasi kwenye mitandao ya kijamii, ni ile ambayo baba yake aliitoa katika kipindi ambacho mjadala wa Katiba Mpya ulipamba moto.

Mwanasiasa huyo alijiapiza kuwa ikiwa “Katiba mpya yenye muundo wa Serikali Tatu itapita, nitaingia mstuni.”

“Sasa imetosha. Nawaomba wamuache baba yangu. Kama alihukumiwa tangu akiwa hai, basi huu sasa uwe muda wa kumuombea ili aweze kupumzika kwa salama,” ameeleza kwa sauti ya unyonge.

Amesema, “Nawaomba wananchi wenzangu, waachane na maneno hayo. Yanaumiza familia. Tumuache Mungu atoe hukumu yake juu yake.”

Maneno mengine ambayo yanakumbukwa kwa Komba ni pale aliposema, “Warioba shida. Shida. Shidaaaa.”

Nukuu nyingine ambayo Komba ametwishwa katika mitandao ya kijamii ni ile inayosikika akisema, “…Chadema haitochukua madaraka wakati bado nikiwa hai.”

Wanaochangia mijadala hiyo wanaonyesha kufurahishwa na kifo chake kwa kusema, “…Komba amevuna alichopanda.”

Mchangiaji mmoja katika mtandao wa MwanaHALISI Forum amesema, “Komba ameingia msituni na kuliwa na nyoka.”

error: Content is protected !!