July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Komba afa na bendi yake ya TOT

Kundi la wasanii wa muziki wa dansi likiimba wimbo maalum wakati wa kumuaga Kapteni John Komba

Spread the love

KUTOKUWEPO kwa Bendi ya Tanzania One Theatre (TOT) katika shughuli ya kuagwa kwa kiongozi wake, Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba, imedhihirisha kuwa kiongozi huyo amekufa na bendi yake. Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).

Kapteni John Komba alifariki dunia Februari 28, 2015 katika hospitali ya TMJ na kuagwa leo kwenye uwanja wa Karimjee jijini Dar es Salaam, lakini katika vikundi vilivyoimba nyimbo za maombolezo, kundi la TOT halikuwepo.

Katika shughuli hiyo iliyoongozwa na Rais Jakata Kikwete, vikundi ambavyo vilipewa nafasi ya kuimba ni msanii wa nyimbo za injili, Rubi aliyeimba wimbo maalum wa kumuaga Kapteni John Komba.

Wasanii wa filamu na muziki nao walipata kuimba wimbo maalum pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa na kundi la Wasanii wa muziki wa Dansi nao waliimba wimbo maalum wa kumuaga Kapteni John Komba.

Matarajio ya wengi ilikuwa ni kuona bendi ya TOT ikiongoza maombelezo ya kiongozi wake lakini badala yake hakukuwa na hata nafasi ya kuimba wimbo maalum kwa ajili ya kumuaga mpendwa wao.

Haijaweleweka moja kwa moja kuwa inawezekana sababu ya kutoonekana kwa bendi hiyo ni mgogoro uliokuwa unafukuta ndani ya kundi hilo kuwa Kapteni John Komba ameiteka bendi hiyo na kujimilikisha.

error: Content is protected !!