Monday , 22 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa  BREAKING NEWS: Kofi Annan afariki dunia
Kimataifa

 BREAKING NEWS: Kofi Annan afariki dunia

Hayati Kofi Annan enzi za uhai wake
Spread the love

KATIBU Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa (UN) Kofi Annan (80), amefariki dunia asubuhi leo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa zilizopatikana mchana huu, zinaeleza kuwa Annan, aliyekuwa katibu mkuu wa saba wa umoja huo – kuanzia 1996 hadi 2006, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu nchini Uswisi.

Inaelezwa kuwa Annan, raia wa Ghana, aliugua ghafla – juzi usiku, na hali yake kubadilika jana na kupelekwa katika moja ya hospitali maarufu (haikutajwa) na kufariki saa 11.30 alfajiri.

Annan atakumbukwa zaidi kwa kuhuisha “heshima” ya umoja huo, baada ya kurekebisha baadhi ya miundo na kusimamia utekelezaji wa majukumu yake ipasavyo.

Mwaka 2001, alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel (akiwa mshindi sambamba na UN) kwa kile kilichoelezwa kuwa ni “kusimamia Amani ya dunia.” Tuzo za Nobel ni maarufu duniani na hutolewa kwa baadhi ya watu wanaofanya vyema na ipasavyo kusaidia “uhai” wa dunia.

Annan aliyezaliwa Mjini Kumasi, Ghana – Aprili 8, 1938 ameacha mke, Nane na watoto watatu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!