Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Habari Siasa Kodi taulo za kike: Zitto ajenga hoja
SiasaTangulizi

Kodi taulo za kike: Zitto ajenga hoja

Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, amepinga pendekezo la serikali la kurejesha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), kwenye taulo za kike. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea).

Mwanasiasa huyo mashuhuri leo tarehe 21 Juni 2019 bungeni amesema, serikali imefanya haraka kurejesha kodi hiyo huku ikishindwa kuchukua mfano wa mwaka jana wa kupandisha kodi ya mafuta ghafi kutoka nje, ili kulinda viwanda vya ndani ambapo licha ya kutoonesha matokeo, bado imejipa muda.

Kwa mfano huo Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema, serikali imefanya haraka kurejesha VAT kwenye taulo hizo kinyume na mapendekezo yake ya mwaka wa fedha 2018/19 ya kuondoa kodi hiyo.

Akisoma makisio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 tarehe 13 Juni 2019, Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango alisema, serikali imependekeza kurejeshwa kwa kodi hiyo kwa kuwa, kuondoa kodi hiyo hakukupunguza bei ya taulo hizo.

Hata hivyo Zitto amesema, serikali haikupaswa kupima matokeo ya kuondoa kodi hiyo kwa mwaka mmoja na kwamba, wakati kodi hiyo inaondolewa wafanyabiashara wengine walikuwa na mzigo ndani hivyo wasingeweza kupunguza.

Lakini pia amesema, bei hiyo inaweza kuwa imebaki palepale kutokana na shilingi ya Tanzania kuyumba kwa kuwa, taulo hizo nyungi zinatoka nje hususan Marekani.

“Serikali inapaswa kutafakati kwamba, je mwaka mmoja ambao utekelezaji umefanyika, unatosha kipimo sahihi?” amehoji Zitto na kuongeza “kodi imeanza Julai 2018 ambapo kulikuwa na watu wana bidhaa ambazo walinunua hazikuwa na punguzo hilo, lazima watauza kwa bei ile ile.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!