Wednesday , 27 September 2023
Home Kitengo Michezo Kocha Zahera: Naondoka Yanga SC
Michezo

Kocha Zahera: Naondoka Yanga SC

Spread the love

MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, anaumizwa na tabia ya wana Yanga kushindwa kuisaidia klabu yao, na sasa ataondoka. Anaripoti Mwandishi Maalum … (endelea).

Kocha huyo mahiri na aliyeiweka Yanga kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mpaka sasa licha ya kuyakabili mazingira magumu ya kifedha klabuni hapo amesema, msimu wa 2018/19 utapotia nanga, naye atahitimisha ukufunzi wake na klabu hiyo.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari nchini Kocha Zahera ameonesha kukerwa na mamilioni ya washabiki kushindwa kujitoa zaidi kwenye timu yao licha ya kujua kwamba, klabu hiyo ipo kwenye wakati mgumu kifedha.

Mtaalamu huyo ameshangaa kuona Yanga ikiitwa klabu ya wananchi na iliyo na watu wenye fedha na uwezo wa kuinyanyua pale ilipo wakishindwa kufanya hivyo na hatimaye ijiendeshe yenyewe.

“Nimefanya mambo mengi sana kuisaidia timu lakini naona wana Yanga wenyewe hawapendi kujisaidia. Nikimaliza msimu huu naondoka,” amesema.

Kocha huyo amekasirishwa kuona michango ya wanachama na mashabiki wa Yanga ikisuasua na kwamba, hatoendelea tena kutoa msaada katika klabu hiyo baada ya msimu huu kumalizika.

Kukasirishwa kwa Zahera kunatokana na yeye kuanzisha kampeni ya kuichangia klabu hiyo kwa wiki nne sasa ambapo jana ilitangazwa kupatikana jumla ya Sh. 21 milioni ambazo anasema ni fedha kidogo kulingana na ukubwa wa Yanga.

Fedha hizo zilitangazwa na Hafidh Salehe, Mratibu wa Klabu ya Yanga tarehe 21 Februari mwaka huu ambapo alisema, fedha hizo zitatumika kununua wachezaji na kujenga uwanja wa mazoezi.

Zahera amesema Mungu hatoamlaumu kwa uamuzi ataochukua kwa kuwa, hawezi kuendelea na Yanga katika mazingira haya.

“Kinachonishangaza zaidi mashabiki na wanachama wao wanalalamika tu timu inapofungwa, sasa nawaomba wajipange ni jinsi gani watayaepuka maumivu kila mara timu ikicheza wapende kujisaidia wenyewe,” amenukuliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMichezo

Ukiwa na Meridianbet ni rahisi kuwa milionea

Spread the love  CARABAO Cup raundi ya 3 Uingereza inaendelea na mechi...

Michezo

Jezi ya Samatta iliyoifunga Liverpool kuuzwa Genk

Spread the love  KLABU ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imeamua kuanza...

BiasharaMichezo

Hii ndio historia ya El-Clasico, derby bora zaidi duniani

Spread the love  KILA nchi ina vilabu viwili hasimu na pinzani nje...

BiasharaMichezo

Piga pesa kupitia Derby ya London Kaskazini kwa kubadhiri na Meridianbet

Spread the love NAJUA umesikia na unazijua Derby nyingi kutoka jiji la London,...

error: Content is protected !!