July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Yanga: Tulitaka kuwaonesha sisi ni wakubwa

Nasriddine Nabi, Kocha wa Yanga (katikati)

Spread the love

 

MARA baada ya kuondoka na ushindi wa bao 1-0. kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mohammed Nabi, amejitamba kwa kusema kuwa ushindi huo, umewaonesha watu kwamba Yanga ni kubwa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo ulipigwa kwenye dimba la Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuanzia majira ya saa 11 jioni na kuhudhuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu.

Ikiwa ni mchezo wake wa kwanza dhidi ya Simba toka atue nchini Aprili 2021, Nabi alisema kuwa, kwenye mchezo wa leo walitaka kuonesha kuwa klabu hiyo ni kubwa licha ya kupitia baadhi ya changamoto, kwenye kipindi cha nyuma.

“Nashukuru kwa timu zote kwa mchezo mzuri, mechi ya leo tulitaka kuonesha ni jinsi gani Yanga ni kubwa pamoja na matatizo waliyopata kwenye kipindi cha nyuma.” Alisena Nabi

Aidha kocha huyo alisema kuwa sio mara ya kwanza kukutana na Simba, kwani alishacheza nao kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa, akiwa na kikosi cha Al Merreikh ya Sudan.

“Sio mara ya kwanza kucheza na Simba, nilivyokuwa sudan nilkutana nao kwenye Ligi ya Mabingwa na niliangalia ubora wao pamoja na mapungufu yao na wachezaji nilio nao.”

“Tusibweteke kwenye hili najua kuna fainali na watakuja kwa hasira.” Aliongezea

Bao la Yanga kwenye mchezo wa leo lilipachikwa kwenye dakika ya 11, kupitia kwa kiungo wake Zawadi Mauya.

Matokeo hayo yalishindwa kuifanya Simba kutangazwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kufuatia kukosa alama tatu.

Kwa upande wa kocha wa Simba Didie Gomes mara baada ya kupoteza mchezo huo alionesha kusikitishwa na matokeo hayo, hasa kipindi cha baada ya kukili kucheza vibaya.

“Ninachoweza kusema kuwa leo najisikia huzuni, tumesikitishwa na matokeo, tuliruhusu kona nyingi kipindi cha kwanza labda kwa kuwa tulifanya makosa mengi.” Alisema Didie

Sasa mafahari wawili hao watakwenda kumenyana tena kwenye fainali ya kombe la Shirikisho, Kigoma tarehe 25 Julai 2021.

Didier Gomes kocha wa Simba

 

 

error: Content is protected !!