May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Yanga amtimua nahodha wake kwa utovu wa nidhamu

Lamine Moro, Nahodha wa Yanga

Spread the love

NAHODHA Mkuu wa kikosi cha Yanga, Lamine Moro ameondolewa kwenye timu hiyo na Kocha Nasriddine Nabi, baada ya kuonesha utovu wa nidhamu, wakati timu ilipokuwa kambini Ruangwa wakijiandaa na mchezo wa Ligi dhidi ya Namungo FC. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo ulipigwa jana na kumalizika kwa suluhu kwenye Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa, mkoani Lindi.

Taarifa zinaeleza kuwa, nahodha huyo ameondolewa kikosini na kurudishwa jijini Dar es Salaam mara baada ya kutokea sintofahamu baina yake na kocha Nabi, jambo ambalo lilionekana siyo afya ndani ya kikosi hiko.

Nasriddine Nabi, Kocha wa Yanga (katikati)

Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amethibitisha nahodha huyo kuondolewa kikosini, huku akieleza sababu kushindwa kufika mazoezini kama kocha anavyotaka licha ya yeye kuwa majeruhi.

“Kocha ameweka utaratibu ambao wachezaji wote wanapaswa kufuata, kwamba hata wale wagonjwa wanapaswa kufika eneo la mazoezi kwa ajili ya kupata ripoti ya pamoja na kuangaliwa na madaktari, lakini Lamine hafanyi hivyo na hata alipoitwa kwenye kikao cha manahodha wote hakutokea bila taarifa yoyote jambo ambalo limeonesha mfano mbaya kwa wengine,” alisema Bumbuli.

Mara baada ya kurudishwa Dar es Salaam, kesi ya mchezji huyo itasikilizwa na uongozi wa Yanga pale timu itakaporudi kutoka Dodoma kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania siku ya Juamtano tarehe 19 Mei, 2021.

error: Content is protected !!