January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Yanga amtetea kipa wake aliyefungwa penati 9

Cedric Kaze, kocha msaidizi wa Yanga

Spread the love

 

KOCHA wa klabu ya Yanga, Cedric Kaze amemtetea mlinda mlango wake Erick Johora aliyeingia kuchukua nafasi ya Aboutwalib Mshery na kufungwa penati tisa kwenye mchezo dhidi ya Azam FC, kwa kusema kuwa wakati wa mazoezi kujiandaa na mchezo huo, mlinda mlango huyo alikuwa bora kuliko mwenzake. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza wa kombe la Mapinduzi ulipigwa leo tarehe 1o Januari 2022, majira ya saa 10:15 kwenye dimba la Uwanja wa Aman uliopo visiwani Zanzibar.

Wakati wa dakika 90 za mchezo Yanga ilimuanzisha mlinda mlango wao kinda waliomsajili kutoka klabu ya Mtibwa Sugar Aboutwalib Mshery na baadada ya dakika kuyoyoya huku timu hizo zikiwa hazijafungana, kocha wa klabu ya Yanga Cedric Kaze akaamua kufanya mabadiliko kwa kumtoa mshery na kumuingiza Johora kwa ajili ya mikwaju ya penati.

Katika mikwaju yote tisa iliyopigwa na wachezaji wa Azam FC kwenye mchezo huo, Johora hakufanikiwa kudaga hata moja licha ya kuingia Uwanjani kwa ajili ya jukumu hilo.

Erick Johora mlinda mlango namba tatu wa klabu ya Yanga

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, akihojiwa kupitia kituo cha Azam TV, Kaze alisema kuwa kitu hicho walikuwa wamekipanga toka wakiwa mazoezi kujiandaa na mchezo huo, lakini kwa bahati mbaya mabadiliko hayo hayakuza matunda.

“Ni kwaida kitu ambacho tulikuwa tumekipanga kwenye mazoezi, yeye ndio alikuwa anaonekana anaweza zaidi lakini ni mabadiliko ambayo hayakuza matunda.” Alisema Kaze

Mlinda mlango huyo alisajiliwa na Yanga kwenye dirisha kubwa la usajili mwezi Agosti akitokea kwenye klabu ya Aigle Noir ya nchini Burundi ambapo alikuwa akicheza soka la kulipwa.

Azam FC ilifanikiwa kuwaondosha Yanga kwa jumla ya mikwaju ya penati 9-8, kufuatia timu hizo kumaliza dakika 90 za mchezo huku zikiwa hazijafungana.

error: Content is protected !!