Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Kocha Yanga afunguka usajili wa msimu ujao
Michezo

Kocha Yanga afunguka usajili wa msimu ujao

Spread the love

Nasreddine Nabi kocha mkuu wa kikosi cha Yanga , amefunguka mipango yake ya usajili kuelekea msimu ujao wa mashindano huku akikili kuhitaji mlinzi mmoja wa kati ili kuimalisha kikosi chake. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Nabi ameyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, dhidi ya Ruvu Shooting uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, na Yanga kufanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 3-2.

Nabi amesema kuwa ameshawambia viongozi wa Yanga kuwa, waandae listi ya usajili wa ajili ya msimu ujao na yeye atatoa mapendekezo ya idara gabi ndani ya uwanja anayotaka ifanyiwe kazi, huku akikili kuihitaji beki mmoja wa kati kwenye kikosi chake.

“Niliwaambia viongozi waandae timu ya usajili, iliwatafute wachezaji, ila ni kweli nataka waongeze beki mmoja wa kati.” Alisema Nabi

Aidha kocha huyo aliongezea kuwa atatoa mapendekezo yake kwa uongozi wa klabu hiyo, maeneo gani anyaotaka yafanyiwe kazi kwenye dirisha la usajili ili wachukue wachezaji wazuri.

Lazarou Kambole, mshambuliaji wa Kaizer Chiefs

“Na nitawaambia kuwa natafuta wachezaji kwenye eneo gani la kiwanja, na wao watasema na kuchukua wachezaji wanaofaa.” Aliongezea Nabi

Kocha huyo anayaesema hayo huku tayari uongozi wa klabu hiyo, umeshamalizana na mlinzi wa kulia Djuma Shabani wa klabu ya As Vita kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Wakiwa wamemalizana na mchezi huyo, katika kuimalisha eneo la ushambuliaji kwa msimu ujao, Yanga waliingia kwenye mazungumzo na klabu ya Kaizer Chiefs, kwa ajili ya kutaka huduma ya mshambuliaji Lazorious Kambole.

Mitandao mbalimbali ya michezo ndani ya bara la Afrika, iliripoti kuwa klabu ya Kaizer Chiefs walishakubaliana na Yanga kumchukua mchezaji huyo kwa mkopo, lakini wakashindwana kwenye maslai binafsi baina ya Yanga na mchezaji.

Taarifa zinaelezakuwa mchezaji huyo ambaye ni raia wa Zambia, analipwa kiasi cha shilingi 18 milioni kama mshahara kwa mwezi ndani ya Kaizer chiefs, na kuitaka klabu ya Yanga Yanga kumlipa kiashi cha shilingi 23 milioni, kama shahara kwa mwezi jambo ambalo hawakuwa tayari.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!