Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Michezo Kocha wa zamani Simba, Azam atua Mtibwa
Michezo

Kocha wa zamani Simba, Azam atua Mtibwa

Spread the love

 

TIMU ya Mtibwa Sugar ya Morogoro nchini Tanzania, imemtambulisha Omog Joseph Marious (49), raia wa Cameroon kuwa kocha mkuu wa timu hiyo. Anaripoti Mitanga Hunda, TUDARCo … (endelea).

Omog aliyewahi kuzifundisha timu za Simba na Azam FC za Tanzania kwa nyakati, ametambulishwa jana Ijumaa, tarehe 24 Septemba 2021.

Katika kurasa zake za kijamii cha Mtibwa, wamewekwa picha za Omog na kuandika “tunayofuraha kumtambulisha kwenu kocha wetu mpya Omog Joseph Marious.”

Joseph Omog

“Ujuzi wake ukichanganya na ujuzi wa kikosi chetu na sukari yetu bora nchini mambo yatakuwa matamu sanaaa..!.”

Omog aliifundisha Simba kwa mwaka mmoja katika msimu wa 2016/17 akianza Azam FC yenye makazi yake Chamanzi-Mbagala jijini Dar es Salaam kati ya 2013 hadi 2015.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!