October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kocha wa Simba aomba radhi

Kocha msaidizi wa Simba, Thiery Hitimana

Spread the love

 

KOCHA msaidizi wa Simba, Thiery Hitimana ameiomba radhi klabu ya Mtibwa sugar kwa kile kilichotokea baina yake na viongozi wa timu hiyo. Anaripoti Hunda Mintanga – TUDARCo … (endelea).

Hitimana ambaye ni raia wa Rwanda amejiunga na klabu ya Simba kwa muda kwa ajili ya michezo ya kimataifa kwani kocha mkuu wa Simba, Dider Gomez hana leseni ya kimataifa ‘CCL PRO’ inayomruhusu kushiriki mechi hizo.

“Mtibwa waligharamia kila kitu mpaka nafika nchini ila baada ya kuanza mazoezi nao nikapigiwa simu na maboss wa Simba wakinihitaji nikafanye kazi na Gomez, nikakubaliana nao kwa sababu ni mtu ambaye tumewahi kufanya nae pamoja tukiwa Rayon Sport.

“Mtibwa wana rasilimali nzuri ya wachezaji hivyo naamini kocha atayekuja atafurahia na kufanya vizuri zaidi kwenye ligi.

“Hivyo ninawaomba yaishe na wafungue ukurasa mpya kwani Mtibwa ni nyumbani kwangu,” amesema.

error: Content is protected !!