January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha wa Simba amzungumzia Ajibu, amtakia kila la kheri

Spread the love

 

KOCHA mkuu wa klabu ya Simba Pablo Martin amemtakiwa kila la kheri mchezaji Ibrahim Ajibu mara baada ya kujiunga na Azam Fc kwenye dirisha dogo la usajili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Ajibu alijiunga na Azam Fc siku ya jana tarehe 30 Desemba 2021, kwa mkataba wa mwaka mmoja mara baada ya mktaba wake kuvunjwa na klabu ya Simba kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo tarehe 31 Desemba 2021, kuelekea mchezo dhidi ya Azam Fc siku ya kesho, kocha huyo alisema kuwa ajibu ni mchezaji mzuri na mwenye kipaji kikubwa lakini amechukua maamuzi hayo kwa kuangalia kiwango chake.

“Ajibu ni mchezaji mzuri mwenye kipaji kikubwa, lakini huu mpira kama kocha lazima nifanye maamuzi kwa kuangalia kiwango cha mchezaji.” Alisema kocha huyo

Ajibu ambaye ameondoka ndani ya klabu ya Simba mara baada ya kudumu kwa miaka nane, katika vipindi tofauti tofauti toka alipopandishwa kutoka kwenye timu ya vijana mwaka 2013, akiwa na umri wa miaka 17.

Aidha kocha huyo aliendelea kusema kuwa anamtakia kila la kheri mchezaji huyo kutokana na mchezaji huyo kuwa na kipaji kikubwa na licha ya kusisitiza kuwa kuna muda unahitajika kuwa na vitu vya ziada.

Nashukuru kwa muda aliyoutumia na mimi na namtakia kila la kheri kwenye kazi yake”

“Ni mchezaji mzuri ila kuna muda kwenye mpira unahitaji vitu vya ziada.” Alisema Pablo

Usajili huo wa Azam Fc unamfanya Ajibu kuwa mchezaji wa tano nchini kucheza klabu zote tatu kubwa katika soka la Tanzania.

Wachezaji wengine waliocheza timu zote tatu ni Mrisho Ngassa, Deogratius Munishi “Dida”, Amri Kiemba, na Gadiel Michael.

error: Content is protected !!