December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Simba: Yanga walikuwa wanazuia

Spread the love

KOCHA wa Simba, Sven Vandebroeck amesema “kuLikuwa  na timu moja inacheza mpira na nyingine inazuia, nawapongeza wachezaji wangu kwa kucheza vizuri na ninafuraha kwa kile walichokionesha.” Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Sven amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Yanga dhidi ya Simba uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Aidha kocha huyo ameendelea kusema kuwa kipindi cha kwanza hakikuwa kizuri kwa upande wao kwa sababu kasi ya mchezo ilikuwa chini lakini pia mwamuzi alisababisha kutokea kwa jambo hilo

“Kipindi cha kwanza hatukuwa na hali nzuri na mwamuzi alikuwa anatuzuia mara kwa mara lakini kipindi cha pili tulimiliki kiufundi na nguvu” aliongezea kocha huyo.

Bao la kusawazisha la Simba lilifungwa dakika ta 86 na beki wake raia wa Kenya Josh Onyango kwa mpira wa kona mara baada ya Yanga kutangulia katika dakika 31′ kwa bao lilifungwa na Michael Sarpong kwa njia ya penati.

Kwa matokeo haya Simba itaendelea kubakia nafasi ya tatu ikiwa na alama 20 nyuma ya Yanga yenye pointi 24 kwenye nafasi ya pili.

error: Content is protected !!