Thursday , 23 March 2023
Home Kitengo Michezo Kocha Simba: Tunahitaji kuwa bora ili tupate matokeo
MichezoTangulizi

Kocha Simba: Tunahitaji kuwa bora ili tupate matokeo

Didier Gomes kocha wa Simba
Spread the love

 

MARA baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-0, dhidi ya Kaizer Chiefs kocha mkuu wa kikosi cha Simba Didier Gomes ameonekana kutofurahishwa na matokeo na kudai kuwa kama wanataka kufuzu kwenye hatua ijayo wanahitaji kuwa bora zaidi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa robo fainali ya kwanza Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ulipigwa jana kwenye uwanja wa FNB uliopo Johannesburg, nchini Afrika Kusini.

Gomes amefunguka hayo mara baada ya mchezo kumalizika huku akionesha kuwa na matumaini ya kupata matokeo kwenye mchezo ujao ambao utapigwa Jumamosi Tarehe 22 Mei 2021, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

“Jambo lolote linawezekana kwenye mpira, hatujafurahia matokeo lakini bado tuna matumaini, ni muhimu sana kuamini kwamba tunaweza kubadili matokeo, lakini kama tunataka kupata matokeo kwenyue mchezo wa marudiano lazima tuwe bora Zaidi,” alisema Gomes

Kwenye mchezo huo wa marudiano Simba inatakiwa kupata ushindi kuanzia mabao 5 na kuendelea bila kuruhusu wavu wao kuguswa.

Kwenye mchezo wa kwanza Kaizer Chiefs walianza kuandika bao la kwanza kwenye dakika ya 6, kupitia kwa Eric Mothoho aliyefunga kwa njia ya kichwa mara baada ya kuunganisha kona na bao la pili lilifungwa na mshambuliaji wao Samir Nurkovic na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Simba ikiwa nyuma kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili kiliporejea Simba ilionekana kumiliki mpira kwa asilimia kubwa hasa eneo la kati kati ya Uwanja, licha ya Kaizer Chiefs kuonekana kuwa na hatari zaidi wanapofika kwenye eneo la mwisho la Simba kwa mashambulizi ya kushtukiza na dakika ya 56 Nurkovic tena aliwaandikia wenyeji hao bao la tatu na kisha dakika ya 63, Leornado Castro akaitimisha kalamau ya bao la nne.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Habari MchanganyikoTangulizi

Rais Samia ampandisha cheo RPC wa Dar

Spread the loveMKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, amesema...

Habari za SiasaTangulizi

Wanachama 384 CUF watimkia Chadema, Mbowe awapokea, Kambaya ndani…

Spread the loveJUMLA ya wanachama 384 wanachama wa Chama cha Wananchi CUF...

error: Content is protected !!