June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Simba: Sina presha, nimeshawasoma Yanga

Didier Gomes, Kocha wa Simba

Spread the love

 

KOCHA wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam nchini Tanzania, Didier Gomes amesema, hana presha kuelekea mchezo wa fainali wa kombe la shirikisho dhidi ya watani zao Yanga. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Fainali hiyo, itachezwa kuanzia saa 9:30 alasiri kesho Jumapili, tarehe 24 Julai 2021, katika Uwanja wa Lake Tanganyika, mkoani Kigoma huku Simba akiwa bingwa mtetezi wa michuano hiyo.

Licha ya kufungwa na Yanga bao 1-0, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Gomes akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, amesema hawezi kuwa na presha kwenye mchezo huo kwani amejifunza kupitia mchezo uliopita ambao walikutana.

“Siwezi kuwa na presha na mchezo huu kwani nimeshawasoma Yanga kupitia mchezo uliopita na nimeona uzuri wao na mapungufu yao pamoja na makossa tuliyoyafanya.”

“Ni lengo letu kutwaa kombe hili na tukifanya hivyo, tutakuwa tumefanikiwa kwa msimu huu,” amesema Gomes.

Gomes amesema mpaka sasa wanajivunia kutwaa mataji manne ya Ligi Kuu Tanzania Bara, na kuwa ni muhimu kwa Simba kutwaa taji hilo ili kumaliza msimu vizuri na kuwapa faruha mashabiki.

“Kwanza tumeshinda mataji manne mfululizo ya ligi kuu ni muhimu sana kwa Simba kulichukua taji hili na tunataka kumaliza msimu huu vizuri na tunataka kufanya mashabiki wetu wafurahi,” amesema

Kocha huyo toka atue nchini Januari 2021, kujiunga na Simba, Gomes amekutana na Yanga kwenye michezo mitatu na kuambulia sare kwenye mchezo mmoja tu, huku akipoteza michezo miwili.

Gomes ataiongoiza Simba kwenye fainali yake ya kwanza toka alipochukua mikoba ya kukinoa kikosi hiko akitokea nchini Sudan.

error: Content is protected !!