November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Simba, Cambiasso, Matola mbaroni kwa dawa za kulevya

Kocha wa makipa wa Klabu ya Simba SC. Muharami Said Sultan

Spread the love

 

JUMLA ya watuhimiwa 11 wamekamatwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) ikiwamo Kocha wa makipa wa Klabu ya Simba SC. Muharami Said Sultan (40) kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya Hereoin. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mbali na Muharami ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu ya Simba SC. mamlaka hiyo pia imemkamata Mfanyabiashara Kambi Zubeir Seif (40) ‘Cambiasso’ ambaye ni mmiliki wa Kituo cha Cambiasso Sports Academy kilichopo Tuangoma- Kigamboni kinachojihusisha na ukuzaji wa vipaji kimichezo.

Cambiasso pia ni mmiliki wa Kampuni ya Safia Group of Companies ambayo inamiliki magari ya kusafirisha abiria ‘daladala’ kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoa wa Pwani.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 15 Novemba, 2022 na Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo, Gerald Kusaya amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kutokana na operesheni iliyofanywa kuanzia Oktoba na mwanzo mwa Novemba mwaka huu.

Amesema DCEA kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vilifanya operesheni meneo mbalimbali nchini na kukamata jumla ya kilo 34.89 za dawa za kulevya aina ya heroin pamoja na biskuti 50 zilizotengenezwa kwa kutumia dawa ya kulevya aina ya bangi kama moja ya malighafi.

Mfanyabiashara Kambi Zubeir Seif (40) ‘Cambiasso’

Cambiasso pamoja na Muharami ni mojawa ya watuhimiwa tisa waliokutwa na dawa za kulevya aina ya Hereoin.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa na wanaendelea kuhojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani ni Said Abed Matwiko (41) mkazi wa Magole ‘A’ kivile ambaye ni fundi seremala; Maulid Mohamed Mzungu (54) – mkazi wa Kamegele Kisemvule ambaye ni mkulima mwenye undugu na mtuhumiwa Muharami.

Wengine Mfanyabiashra John Andrew John maarufu kama Chipanda (40) mkazi wa Magore Kitunda ni ambaye pia ana jukumu la kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka Cambiasso Sport Academy.

Mfanyabiashara Rajabu Mohamed Dhahabu (32) – mkazi wa Tabata Segerea, Mkulima Seleman Matola Said (24) mkazi wa Temeke Wailes ambaye ni mtoto wa dada yake mtuhumiwa Kambi Zubeir Seif ‘Cambiasso’.

Pia amewataja wafanyabiashara Hussein Mohamed Pazi (41) mkazi wa Kibugumo Kigamboni na Ramadhani Rashid Chalamila (27) mkazi wa Mzinga- Kongowe.

error: Content is protected !!