May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Simba atamba kuingamiza Polisi Tanzania

Seleman Matola kocha msaidizi wa klabu ya Simba

Spread the love

 

KOCHA msaidizi wa klabu ya Simba, Seleman Matola amejinasibu kikosi chake kuwa tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Tanzania Bara, dhidi ya Polisi Tanzania, huku akitamba na rekodi ya kuwafunga kwenye michezo mitatu iliyopita. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza majira ya saa 10 jioni, ambapo kikosi cha Polisi Tanzania kitakuwa nyumbani.

Akielezea hali za wachezaji kuelekea mchezo huo, Matola alisema wachezaji wote wapo tayari, huku akifunguka kuwa dhamira yao ni kushinda michezo mitatu ijayo ya Ligi ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa taji la Ligi Kuu msimu huu wa 2020/21.

“Kikosi kipo kamili wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri, tunawaheshimu Polisi mara zote tukikutana wanatupa ushindani mkubwa lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” alisema Matola.

Kikosi cha Simba kikifanya mazoezi kwee Uwanja wa Nyamagana

Matola aliongezea kwa kusema kuwa katika michezo mitatu iliyopita dhidi ya Polisi kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, walifanikiwa kuondoka na ushindi kwenye mechi zote, licha ya kutambua mchezo wa kesho kuwa mgumu.

Kwa upande wa naohodha msaidizi wa kikosi hiko, Mohammed Hussein, alisema wao kama wachezaji malengo yao ni kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa kesho, ili kujitengenezea mazingira mazuri katika kutetea taji lao la ubingwa.

Simba inaingia kwenye mchezo wa kesho, huku ikitafuta pointi 10, ili kutangazwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa sasa Simba wapo kileleni wakina na pointi 67, baada ya kucheza michezo 27, huku nafasi ya pili wakiwa klabu ya Yanga wakiwa na pointi 64 baada ya kucheza michezo 30.

error: Content is protected !!