August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Simba ashtuka, Okrah, Phiri wapewa kazi nzito

Spread the love

 

MARA baada ya kupoteza mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu, kocha mkuu wa klabu ya Simba Zoran Maki ameanza tena kulifanyia kazio eneo lake la ushambuliaji katika kutafuta makali kuelekea msimu ujao wa mshindano. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Simba walipoteza mchezo huo wa kujipima nguvu kwa mabao 2-0, dhidi ya Haras El Hodoud ya nchini Misri ambapo timu hiyo imekita kambi ya wiki tatu kujian daa na msimu ujao.

Mchezo huo ambao ulikuwa watatu kwa Simba toka walipoanza mazoezi wiki moja iliyopita, na imekuwa mechi ya kwanza kupoteza mara baada ya kufanya vizuri kwenye mchezo uliopita.

Akizungumza kutokea nchini Misri mara baada ya mchezo kumalizika, kocha mkuu wa klabu ya Simba Zoran Maki sbbu ya kupoteza mchezo huo dhidi ya wapinzani hao ni kutokana kutokuwa vizuri kwenye eneo lao la kiungo kwa kutengeneza nafasi.

“Hatukuwa bora kwenye kiungo, hatukutengeneza nafasi ukiachilia ile moja finyu.” Alisema Zoran

Kwenye eneo hilo la kiungo tayari kwenye dirisha hili la usajili klabu ya soka ya Simba, imeliongezea nguvu kwa kumsajili kiungo kutoka nchini Ghana Agustine Okrah ambapo kocha huyo itamlamzimu kurudi tena kwenye Uwanja wa mazoezi na kumpatia majukumu mapya, yatakayoweza kuleta matokeo chjanya kwenye timu hiyo.

Ukiacha eneop hilo tu, lakini pia klabu hiyo imeshaongeza tena nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji kwa kumsajili Moses Phiri ambaye pia itamalazimu kocha huyo kumnoa sambamba na viongo hao, ambao wanatengeneza muunganiko katika sehemu ya mbele.

Maelezo ya kocha huyo yameomnesha kwa namna gani amezamilia kuhakikisha timu hiyo inatengeneza nafasi za kutosha kwenye michezo yake, ambayo itawakikishia kupata ushindi.

Kwenye msimu uliopita Simba ilionekana kuwa kwenye wakati mgumu hasa kwenye eneo la ushambuliaji kutokana kwa kutokuwa na mabao ya kutosha kutoka kwa washambuliaji wake watatu, John Bocco, Meddie Kagere na Chris Mugalu ambao mara kwa mara walikuwa wakisumbuliwa na majeruhi.

Aidha kocha huyo aliendelea kwa kufunguka kuwa. Licha ya kupoteza mchezo huo lakini hali ya uwanja hasa kwenye eneo la kucheza halikuwa vizuri lakini kwa upande wake sio sababu ya kupoteza mchezo huo.

“Eneo la kuchezea halikuwa vizuri, lakini hiyo haiwezi kuwa sababu, hatukutengeneza tu nafasi na haikuwa mechi nzuri kwetu.” Alisema Zoran

Kwa mujibu wa Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally ambaye yupo sambamba na timu nchini Misri alisema kuwa kwa sasa Simba imebakisha michezo miwili ya kujipima nguvu ambao kwenye siku za hivi karibuni watatoa taarifa watacheza na nani.

Ikumbukwe wakati timu hiyo inaelekea nchini humo, wakiwa na kocha wao mpya Zoran alibainisha kwa uongozi kuwa atahitaji michezo isiyopungua mitano ya kirafiki katika kukipima kikosi chake.

Tayari mpaka nsasa Simba imeshacheza michezo mitatu, ambapo katika hiyo mchezo wa kwanza walienda sare ya bao 1-1, dhidi ya Ismailia, na mchezo wa pili walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 6-0, dhidi ya Al-Akhood na mchezo wa tatu wamepoteza kwa mabao 2-0.

Klabu hiyo ipo kwenye siku za mwisho kumalizia maandalizi ya yao nchini Misri, kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam, ambapo itashuka dimbani Agosti 8 mwaka huu kwa ajili ya mchezo kwenye tamasha la Simba.

Na mara baada ya hapo timu hiyo itaingia mawindoni kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi wa Ligi wa ngao ya hisani dhidi ya Yanga utakaopigwa Agosti 13 mwaka huu, kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!