May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Simba ahaidi Burudaani dhidi ya Yanga

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba

Spread the love

 

KOCHA Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kuwa kikosi chake kesho kimepanga kwenda kuonesha burudani kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utachezwa kesho majira ya saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo wa kesho, Matola amesema kuwa licha ya mechi hiyo kuwa na presha lakini wao kama Simba watahakikisha wanacheza mpira wao wa kila siku ambao utakuwa na burudani kwa mashabiki wao.

“Mechi hizi zinakuwa na presha kubwa, sisi tunataka tukaonyeshe burudani kwa kucheza mpira wetu wa kila siku na hatutaki kuwa tofauti kwa kucheza kwa kubutua,” alisema Matola

Aidha kocha huyo amesema kuwa mpaka sasa kwenye kikosi chake hakuna majeruhi ya aina yoyote na wachezaji wote wapo sawa.

Pia Matola amejitanabaisha kuwa wachezaji waliokuwa kwenye kikosi hiko wanauzoefu wa kutosha licha ya mchezo huo kuwa katika presha kubwa.

error: Content is protected !!