July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Pitso wa Al Ahly aachana na klabu yake

Pitso Mosimane

Spread the love

PITSO Mosimane ameachana na miamba ya Misri Al Ahly kwa makubaliano, miezi mitatu baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kama kocha mkuu. Anaripoti Mwandishi Wetu kwa Msaada wa Mashirika ya Kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). 

Raia huyo wa Afrika Kusini aliiongoza klabu hiyo ya Cairo kunyakua mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kujiunga nayo mwaka 2020, lakini timu yake ilipoteza fainali ya msimu huu kwa Wydad Casablanca.

Mosimane mwenye umri wa miaka 57 pia alifanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu mfululizo katika Kombe la Dunia la Klabu, ikiwa ni pamoja na michuano ya 2021 iliyochezwa Februari.

Uamuzi wa kuachana nao ulifikiwa kufuatia kikao kilichofanywa na rais wa Al Ahly Mahmoud El Khatib, mwenyekiti Yassin Mansour, mjumbe wa bodi Hossam Ghaly na wajumbe wengine wa kamati ya mipango ya klabu hiyo.

Taarifa ilisema kuwa klabu hiyo inatamani Mosimane aendelee na Ahly, lakini kocha huyo wa zamani wa Afrika Kusini na Mamelodi Sundowns aliomba kuondoka katika klabu hiyo.

“Wakati wa mkutano huo, wote waliamua kwamba aendelee na ariri aliyokuwa nayo Al Ahly kutokana na mafanikio aliyoweza kuyatimiza,” taarifa ya Al Ahly ilisema.

“Lakini, wakati wa mkutano ambao ulifanyika hapo awali, Mosimane aliomba kuondoka. “Uamuzi wa Mosimane ulijadiliwa na ikaamuliwa kuidhinisha ombi lake la kuachana na klabu.”

Mosimane alikuwa amekubali kusaini mkataba mpya mwezi Machi, ambao ungemwezesha kusalia Ahly hadi 2024.

Samy Komsan amepewa nafasi ya kuongoza kwa muda kwa michezo ijayo ya kikosi cha kwanza katika Ligi Kuu ya Misri na Kombe la Misri.

error: Content is protected !!