
Spread the love
Mara tu baada raia huyo wa Ubelgiji kutangazwa ameesema hana habari na watani zao wa jadi Yanga, yeye mipango yake ni kuifanya Simba kuwa Big Team Afrika (timu kubwa Afrika).
Patrick amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuinoa klabi hiyo huku akisisitiza kuwa atafanya kazi na makocha wazawa.
Katika hafla ya kumtambulisha kocha huyo amesema anaijua Yanga na Azam lakini Simba ndiyo kila kitu kwake.
“Kama nilivyosema naifikiria Simba kuwa moja ya timu kubwa Afrika, tageti yangu ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na kufika mbali mashindano ya kimataifa,” amesema.
Rais wa Simba, Salim Abdallah amesema wamempa mkataba wa mwaka mmoja na atafanya kazi akisaidiana na Masudi Djuma sanjari na Kocha wa viungo ambaye atatajwa siku si nyingi.
More Stories
Namungo yafuzu makundi, yakubali kipigo bao 3-1
Kim Poulsen kutangaza kikosi cha Stars kesho
Chadema yatangaza mchakato mrithi wa Halima Mdee