May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha mpya Simba: Namjua Kagere

Spread the love

 

KOCHA mpya wa timu ya Simba, Didier Gomes amesema kuwa ameifuatilia kwa karibu Ligi Kuu ya Tanzania Bara na kuwafahamu baadhi ya wachezaji ikiwemo Meddie Kagere ambaye alimfundisha alipokuwa kwenye klabu ya Rayol Sport ya nchini Rwanda. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kocha huyo ametua nchini jana na kujiunga na klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili leo Jumapili 24 Januari 2021.

Wakati akijibu swali la mwandishi wa habari kwa namna gani ameifuatilia Ligi Kuu ya Tanzania na kujibu kuwa ameifuatilia Ligi hii kwa muda mrefu kwa kuwa inaendelea kukua taratibu kwa siku za hivi karibuni.

“Naijua na nimeifuatilia Ligi ya Tanzania kwa kuwa ni moja ya Ligi nzuri na inakuwa kila siku na hata hivyo nawajua baadhi ya wachezaji akiwemo Meddie Kagere ambaye nilimfundisha nikiwa nchini Rwanda nikiwa na klabu ya Rayon Sports,” alisema kocha huyo.

Kagere ambaye alikuwa hapati nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha kocha aliyeondoka kutokana na mfumo wake wa kutumia mshambuliaji mmoja na kuamua kumtumia zaidi John Bocco.

Pengine ujio wa Gomes huenda ukampa tena nafasi mchezaji huyo ambaye alikuwa mfungaji bora wa klabu hiyo pamoja na Ligi Kuu kwenye msimu uliomalizika.

error: Content is protected !!