May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Dodoma Jiji: Tutaishangaza Simba kesho

Spread the love

 

KOCHA msaidizi wa kikosi cha Dodoma Jiji, Renatus Shija ameapa kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba kesho kutokana na kuamini katika mbini zake. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa Ligi Kuu utachezwa kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam majira ya saa 1 usiku.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa Habari kocha huyo msaidizi amesema kuwa wamejipanga vizuri kukikabili Simba kesho licha ya kukili kuwa na kikosi kizuri kwa sasa.

“Tumejipanga vizuri kwa mchezo wa Simba kesho najua tupo Dar es Salaam na hapa ndiyo ngome yao kuu, lakini kuna kitu tumekiandaa tunataka tukawashangaze kesho ili tuondoke na pointi tatu katika mchezo huo,” alisema kocha huyo.

Timu hiyo inakwenda kucheza na Simba huku ikiwa imetoka kutoa sare kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC mara baada ya kufungana mabao 2-2.

Kwa sasa Dodoma Jiji ipo nafasi ya sita kwenye msimamo huku ikiwa na pointi 38 mara baada ya kucheza michezo 27.

error: Content is protected !!