Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Michezo Kocha atoboa siri ya ushindi Biashara United
Michezo

Kocha atoboa siri ya ushindi Biashara United

Spread the love

 

KOCHA wa kikosi cha Biashara United, Moses Odhiambo amesema kuwa ubora wa wachezaji wake ndio siri kubwa ya kupata ushindi dhidi ya Al Ahly Tripoli ya kutoka nchini Misri. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, ulimalizika kwa Biashara United kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mara baada ya mchezo huo, kocha huyo ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars) alifungukuwa kuwa, siri ya kuondoka na ushindi kwenye mchezo huo ni ubora wa wachezaji wake, licha ya kukili kuwa wapinzani wao wanatimu nzuri.

“Wachezaji wangu walikuwa bora, wapinzani wetu wanatimu nzuri, ila niliona kitu cha wachezaji wangu kutaka kushinda mechi hii.” Alisema Odhiambo

Mabao ya Biashara United kwenye mchezo huo, yalipachikwa kambani na Deogratius Mafie, kwenye dakika 40 ya mchezo, huku bao la pili likifungwa na Atupele Green, dakika ya 62 ya mchezo.

Aidha kocha huyo aliendelea kufunguka  kuwa, bado kazi haijamalizika kwa kuwa wanamchezo wa marudiano hivi karibuni.

“Hatujamaliza, kwa kuwa wapinzani wetu wanaonekana kuwa na timu nzuri sana, na wakiwa nyumbani kwa wanakuwa bora sana.” Alisema Kocha huyo.

Mchezo huo wa marudiano wa utapigwa nchini Libya, Oktoba 24, 2021 ambapo Biashara United wanahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili waweze kusonga mbele kwenye hatua inayofuata.

Biashara United wanashiriki michuano hii kwa mara ya kwanza, toka walipopanda kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na kumaliza nafasi ya nne kwenye msimu uliomaliza.

Mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Biashara kitasafiri kuelekea Sumbawanga, ambapo Oktoba 19, 2021 kitashuka dimbani kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!