May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha aliyekaa siku 41 Al Merreikh atua Yanga

Spread the love

 

KLABU ya Soka ya Yanga leo imemtambulisha Mohamed Nasreddine Nabi aliyedumu kwenye kikosi cha Al Merreikh ya Sudan kwa siku 41, kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, ambaye amekuja kuchukua mikoba ya Cedric Kaze aliyetimuliwa hivi karibuni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kocha huyo raia wa Misri amesaini mkataba huo leo tarehe 20 Aprili 2021 kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Jangwani Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa utiaji saini mkataba huo, Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Haji Mfikilwa amesema kuwa kocha huyo ni sahihi kwa kuwa hawazingatii ligi ya nyumbani na wanaamini katika uzoefu wake.

“Ni chaguo sahihi, kwa sababu hatuzingatiii ligi ya nyumbani bali michuano ya Afrika, ni mtu mwenye uzoefu na soka letu la Afrika,” alisema Mfikilwa.

Mohamed Nasreddine Nabi, Kocha wa Yanga

Kocha huyo raia wa Misri, amekuja na msaidizi wake Sghir Hammad ambao wote kwa pamoja wameingia mkataba wa miezi 18.

Mara baada ya kusaini mkataba huo kocha huyo, alisema kuwa amefanikiwa kuiona Yanga ni timu kubwa, ina wachezaji wazuri licha ya kuwa na mapungufu madogo madogo.

Nabi alidumu ndani ya kikosi cha Al Merreikh kwa siku 41, kufuatia kutoa sare ya bila kufungana dhidi ya Simba kwenye mchezo wa kundi A, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Alijiunga na Al Merreikh tarehe 28 Januari, 2021, kuchukua mikoba ya Didier Gomes aliyetimkia Simba na tarehe 7 Machi, 2021 alitimuliwa mara baada ya kutolidhishwa na matokeo ya kwenye mchezo dhidi ya Simba.

error: Content is protected !!