May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Al Ahly aikubali Simba, awataja Miquison, Chama, Mugalu

Spread the love

 

KOCHA Mkuu wa Al Ahly, Pitso Mosimane ametaja wachezaji Luis Miquison, Clatous Chama na Chriss Mugalu kama wachezaji wa kuwachunga kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya Simba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa kundi A, utachezwa kesho majira ya saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo Simba itakuwa inatupa karata yake ya pili baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0, kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya AS Vita Club nchini Congo.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari hii leo kuelekea mchezo wa kesho Pitso amesema kuwa Simba wanacheza vizuri sana na moja ya timu inayocheza kwa kutegemea nguvu ya mashabiki na wana wachezaji wazuri.

“Simba ni timu nzuri na inacheza vizuri pia inawachezaji wazuri kama Luis Miquison ambaye nilimsajili kutoka Msumbuji nilivyokuwa Mamelod Sundown, Chama pia mchezaji mzuri nilimuona tulivyocheza na Zesco,” alisema Pitso.

Kocha huyo hakuishia hapo tu aliendelea kuwataja wachezaji kama Chriss Mugalu na Meddie Kagere kama washambuliaji hatari wanaokipiga kwenye kikosi cha Simba.

Aidha Pitso alisema kuwa ni jambo zuri kwa Simba kupata ushindi kwenye mchezo dhidi ya AS Vita Club kutoka Congo DR na kueleza kuwa na hiyo ndiyo moja ya sababu inayowafanya kuwaangalia kwa jicho la tatu kuelekea mchezo huo siku ya kesho licha ya wao kupania kuchukua pointi tatu.

“Ni jambo zuri kwa Simba kwenda Kinshasa na kushinda dhidi ya AS Vita Club na ni moja ya jambo ambalo tunatakiwa kuwa makini kwa kuwa wanacheza vizuri,” alisema Pitso.

error: Content is protected !!