August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

K’ndon kunufaika na mafunzo ya kilimo

Spread the love

WAKAZI wa Manispaa ya Kinondoni wanatarajiwa kunufaika na mradi wa kituo cha mafunzo ya kilimo, anaandika Pendo Omary.

Akizungumza leo na Mwanahalisi Online ofisini kwake, Salim Msuya, Ofisa Kilimo wa Manispaa hiyo amesema, mradi huo wa Kituo cha Mlolo ulipo kwenye Kata ya Mabwepande, Tarafa ya Kawe utaghalimu jumla ya Sh. 239,522,200 ambazo ni fedha kutoka Halmashauri ya Kinondoni.

“Hivi sasa mradi huu umelipwa kiasi cha Sh. 174,414,245.90 na mkandarasa anayejenga mradi huu ni Kidale Building and Civil Engineering Ltd,” amesema Msuya na akuongeza;

“Mradi huu utawanufaisha vijana, wanawake na makundi mengine wakiwemo wastaafu ambao watapata elimu na mbinu bora za kilimo cha kisasa.

“Wanufaika wataweza kujiongezea kipato na kuwa na uhakika wa chakula kwa mwaka mzima. Hii ni baada ya kupata mafunzo na kuyatumia katika maeneo yao na kuzalisha mazao yenye kiwango na bora,” ameeleza Msuya.

error: Content is protected !!