December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

KMC yapata ushindi wa kwanza dhidi ya Azam

KMC

Spread the love

 

BAADA ya kucheza dakika 450 pasina kuibuka na ushindi wowote katika Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2021/22, timu ya KMC ya Kinondoni jijini Dar es salaam, wameitwanga Azam FC 2-1. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaan … (endelea).

KMC imeibuka na ushindi huo wa kwanza leo Jumapili, tarehe 21 Novemba 2021, katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam na kuwafanya kufikisha pointi tano kati ya michezo sita iliyocheza.

Mchezo huo uliokuwa wa kushambuliana kwa zamu na kushuhudia kila timu ikokosa nafasi za wazi, KMC ilikuwa ya kwanza kuingia wavuni dakika ya 12 kipindi cha kwanza kupitia kwa matheo Anthony.

Hata hivyo, dakika mbili kabla ya kipindi cha kwanza hakujamalizika, nahodha wa Azam FC, Sospeter Bajana aliisawazishia timu yake na kwenda mapumziko 1-1.

Kipindi cha pili kama ilivyokuwa cha kwanza, timu zote zilijitahidi kutengeneza nafasi na kama vile mchezo huo unamalizika kwa sare, Hassan Kabunda aliifungia KMC bao dakika ya 89.

Amefunga bao hilo akiunganisha mpira uliotemwa na mlinda mlango wa Azam, Mathias Kigonya ambaye awali, alishuhudia akipangua michono mingi.

Hiki ni kipigo cha tatu mfululizo kwa Azam FC ambayo imeshuka dimbani mara sita ikiwa na pointi saba huku Yanga ikiongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 16.

error: Content is protected !!