TIMU ya KMC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara imehamishia mchezo wake wa nyumbani dhidi ya klabu ya Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza kama walivyopendekeza baada ya mabadiliko ya ratiba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Mchezo huo namba 70 unatarajiwa kuchezwa 25 Oktoba, 2020 majira ya saa 10 jioni kwenye dimba la CCM Kirumba.
Kwa kawaida KMC hucheza michezo yake ya nyumbani ya Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es Salaam lakini mchezo wao dhidi ya Yanga watauhamishia Mwanza kutokana na kanuni kuruhusu timu kuchagua mechi mbili ambazo watacheza kwenye uwanja wa chaguo lao tofauti na uwanja wa nyumbani.
KMC kwa sasa inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 9, mara baada ya kucheza michezo mitano huku akishinda mechi tatu na kufungwa mbili.
Leave a comment