TIMU ya KMC FC ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imeanza kwa kushindo Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2020/21 kwa kuifunga Mbeya City 4-0. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mchezo huo umechezwa leo Jumatatu tarehe 7 Septemba 2020 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Ushindi huo wa KMC ni mkubwa katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ilianza jana Jumapili kwa michezo saba kati ya tisa.
Katika mchezo mwingine kati ya Kagera Sugar dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera ulimalizika kwa wenyeji kulala kwa bao moja lililofungwa dakika ya 16 na Adam Adam.
Saa 1:00 usiku wa leo, Azam itacheza na Polisi Tanzania katika Uwanja wa Azam Complex Chamanzi jijini Dar es Salaam kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.
Leave a comment