July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

KMC warudisha Dar mchezo wao dhidi ya Simba

Spread the love

 

Klabu ya KMC ya jijini Dar es Salaam, imerejesha mchezo wake dhidi ya Simba jijini Dar es Salaam, kwenye dimba la Benjamin Mkapa, badala ya CCM Kirumba, Mwanza kama ilivyopangwa hapo awali. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo, utapigwa tarehe 7 Julai, 2021, licha ya uongozi wa klabu hiyo kutoeleza sababu za msingi, kurudisha mchezo huo Dae es Salaam.

Licha ya kutumia Uwanja wa Uhuru katika michezo yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara, KMC walitangaza kupeleka michezo yao dhidi ya Simba na Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Katika kutekeleza hilo, mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ambao KMC walikuwa nyumbani dhidi ya Yanga, uliochezwa tarehe 25 Oktoba, 2020, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kikosi hiko chenye maskani yake Kinondoni, Dar es Salaam kimesalia na michezo mitatu kabla ya kukamilika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21, ambayo ni dhidi ya Simba, JKT Tanzania pamoja na Ihefu.

Kwenye mchezo wamzunguko wa kwanza, ambapo timu hizo mbili zilikutana, kwenye Uwanja wa Mkapa tarehe 16 Desemba, 2020, Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

error: Content is protected !!