May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

KMC waitangazia vita Ruvu shooting kombe la FA

KMC

Spread the love

 

MARA baada ya kuvuna pointi nne kwenye michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya Kwanza na Tanzania Prison, kikosi cha Kmc chenye maskani yake Kinondoni, jijini Dar es Salaam kimeingia kambini kujiwinda na mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Ruvu Shooting. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo wa hatua ya 32 bora utapigwa jumamosi ya Januari 29, mwaka huu kwenye dimba la Uhuru majira ya saa 10 jioni.

Kikosi hiko kimeingia kambini siku ya leo jijini Dar es Salaam chini ya kocha wake mkuu Thiery Hitimana ambaye alisema kuwa wanafahamu ugumu wa michuano hiyo ila wanajiandaa vizuri kuhakikisha wanaendelea kusalia kwa kuwa wamejipanga vizuri.

“Tunafahamu ukubwa na ushindani wa michuano hii, lakini kama Timu tumejipanga vizuri kwani mkakati wetu ni kuhakikisha kwamba tunafanya vizuri na kuendelea kushiriki kwenye michuani hii kwa mafanikio, lakini pia tunafahamu kila Timu ambayo inashiriki inahitaji kufanya vizuri hivyo nasisi tumejipanga pia.” Alisema kocha huyo

Kocha huyo ambaye anakwenda kuiongoza Kmc kwenye mchezo wa tatu mara baada ya kujiunga nao siku za hivi karibuni kama kocha mkuu akichukua nafasi ya Habibu Kondo ambaye aliamua kuondoka kwenye klabu hiyo.

Katika michezo miwili ambayo Kmc wamecheza kwenye Ligi Kuu chini ya kocha Hitimana, walifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prison mkoani Sumbawanga na kisha kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya kwanza, mchezo uliopigwa kwenye dimba la Sokoine.

error: Content is protected !!