Monday , 29 May 2023
Home Kitengo Michezo KMC, Alliance wazibwaga Simba, Yanga tuzo Ligi Kuu
Michezo

KMC, Alliance wazibwaga Simba, Yanga tuzo Ligi Kuu

Spread the love

MSHAMBULIAJI Dickson Ambundo wa klabu ya Alliance Accademy na Kocha Mkuu wa KMC, Etiene Ndayiragije wameibuka vinara kwenye tuzo za mwezi Januari zinazotolewa na Bodi ya Ligi baada ya kufanya vizuri kwenye michezo yao. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea)

Ambundo ameibuka kinara kwenye tuzo hiyo baada ya kuwashinda mlinda mlango wa KMC, Juma Kaseja na mshambuliaji wa Coastal Union, Ayoub Lyanga huku kocha Etiene alifanikiwa kuwapiku makocha Malale Hamsini ambaye anakinoa kikosi cha Alliance na Amri Said wa Biashara United.

Ndayiragije amefanikiwa kuiongoza KMC katika michezo 24 ya Ligi Kuu Tanzania Bara toka ilipopanda daraja na kufanikiwa kujikusanyia alama 35 na kushika nafasi ya tano kwenye msimamo.

Washindi wa tuzo hiyo katika msimu huu wa 2018/19 watajinyakulia kitita cha Sh. 1 milioni kutoka kwa mdhamini mkuu Biko Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

NBC Dodoma Marathon yazinduliwa, wakiambiaji 6,000 kushiriki

Spread the loveBENKI ya NBC imetangaza kufanyika kwa mbio kubwa za NBC...

Michezo

Rais Samia anunua tiketi 5000 Yanga vs USM Alger

Spread the loveRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu...

Michezo

Mwenyekiti UVCCM anogesha nusu fainali Kimwanga CUP, Hawa Abdul Rede CUP kwa kishindo

Spread the loveHEKAHEKA za michuano ya kuwania kuingia fainali ya michuano ya...

Michezo

Yanga SC. yatwaa ubingwa wa pili mfululizo

Spread the love  KLABU ya Yanga SC imeweka rekodi ya kutwaa ubingwa...

error: Content is protected !!