March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Klopp awagwaya Leicester City

Spread the love

MENEJA wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp ameonekana kuwahofia dhidi klabu ya Leicester City katika kuelekea kwenye mchezo wao wa ligi kuu nchini Uingereza utakaopigwa siku ya Jumamosi kwenye dimba la King Power. Anaripoti Kelvin Mwaipungu …. (endelea).

Klopp ambaye amechaguliwa kuwania tuzo ya kocha bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya Uingereza amesema kwa sasa Leicester wanaonekana kubadili aina yao ya mchezo, wanacheza vizuri na kwa kujiamini.

“Unaweza kuona kocha Claude Puel anafanya kazi nzuri, amebadilisha jinsi ya kucheza, ni mpira mzuri wanaocheza na kujiamini zaidi. Utakuwa mchezo mgumu kwetu,” amesema Klopp.

Liverpool ambayo mpaka sasa imeshinda michezo yao miwili iliyopita inapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji la Ligi Kuu nchini humo kutokana kuwa na kikosi kizuri na kilichofanya vizuri katika msimu uliomalizika wa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya licha ya kupoteza mchezo wao wa fainali dhidi ya Real Madrid.

error: Content is protected !!