Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Klabu zenye madeni kutoshiriki Ligi Kuu msimu ujao
MichezoTangulizi

Klabu zenye madeni kutoshiriki Ligi Kuu msimu ujao

Spread the love

 

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeelezeka kuwa klabu yoyote ambayo inadaiwa na wachezaji haitoweza leseni na kushiriki michuano mbalimbali msimu ujao ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

TFF imeleza hivyo kupitia taarifa yake iliyotolewa hii leo tarehe 27 Mei, 2021 mara baada ya kufunguliwa kwa maombi ya leseni kwa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu, Ligio daraja la kwanza na Ligi daraja la pili katika msimu wa 2021/22.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa zoezio la urudishwaji wa fomu wa maombi hayo litafungwa tarehe 15 Juni, 2021.

Aidha katika taarifa yao hiyo shirikisho hilo limeleza kuwa kuanzia msimu ujao wa mashindano 2021/21, klabu yoyote ambayo inadaiwa na mchezaji haitapatiwa leseni ya kushiriki Ligi katika ngazi zote.

“Kwa msimu ujao wa 2021/22 klabu yoyote itakayokuwa inadaiwa na mchezaji haitapatiwa leseni ya kushiriki Ligi.” ilieleza taarifa hiyo

Katika hatua nyingine taarifa hiyo ilitoa tahadhari ya timu zitakazoshiriki michuano ya CAF (Ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho) wakufunzi wao wanapaswa kuwa na leseni A na B ya shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika.

“Klabu itakayoshiriki mashindano ya CAF, kocha mkuu ni lazima awe na leseni A ya CAF na kocha msaidizi ni lazima awe na leseni B ya CAF.” Ilimalizia taarifa hiyo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yatoa tamko bungeni sakatala la viboko shuleni

Spread the love  SERIKALI imewaagiza maafisa elimu wa mikoa na wilaya kuratibu...

Habari za SiasaTangulizi

Lema kurejea Machi 3 na sumu ya kuangamiza chawa

Spread the love  HATIMAYE Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia...

error: Content is protected !!