Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Klabu za Ligi Kuu zamlilia JPM
Michezo

Klabu za Ligi Kuu zamlilia JPM

Rais John Magufuli
Spread the love

 

KUFUATIA kifo cha Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, klabu mbalimbali za Ligi Kuu Tanzania Bara zimetuma salamu za rambirambi kila moja ikieleza mguso wake kutokana na msiba huo mzito. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kifo cha Rais Magufuli kilitangwa jana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu na kutangaza siku 14 za maombolezo kuanzia jana tarehe 17 Machi, 2021.

Kupitia kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii klabu hizo zilionesha namna zilivyoguswa na kifo hiko katika nyanja ya kimichezo.

Kwenye ukurasa za mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, klabu ya Simba waliandika wamepokea kwa mshtuko taarifa ya kifo hiko na kutuma salamu za rambirambi kwa Makamo wa Rais Mh. Samia Suluhu pamoja na ndugu na familia.

Kwa upande wa klabu ya Yanga waliandika, wamepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Rais Magufuli na kwa niaba ya wanachama wametuma salamu za rambi rambi kwa makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu.

Nao Azam FC hawakuwa nyuma, mara baada ya kupata taarifa hiyo walituma salamu zao za rambirambi huku wakieleza kuwa wataungana na watanzania wote kuomboleza kifo cha mpendwa wetu, kwa kutambua na kuheshimu mambo makubwa aliyolifanyia Taifa hili kwa muda wote aliohudumu ndani ya Serikali.

Kagera Sugar kutoka Kaitaba, baada ya taarifa ya kifo cha Rais Magufuli walisema kuwa uongozi wao umepokea kwa masikitiko taarifa ya msiba huo na kutoa pole kwa wanamichezo na watanzania wote walioguswa na msiba huu mzito wa Taifa.

Klabu za Mtibwa Sugar pamoja na Biashara United nao hawakuwa mbali kwenye kutoa salamu zao za rambirambi huku kila moja ikionekana kupokea kwa masikitiko taarifa hiyo na kutuma salamu za pole kwa Makamou wa Rais na watanzania kwa ujumla.

Nazo klabu kutoka jijini Mbeya, Ihefu FC na Mbeya City zilionekana kuguswa na kifo hiko na kutuma salamu zao za rambirambi kwenda kwa Makamo wa Rais na watanzania kwa ujumla kufuatia kifo cha Rais Magufuli.

Ihefu FC wao walitoa salamu hizo kupitia bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo na kuungana na watanzania wote katika maombolezo haya.

Coastal Union kwa upande wao waliandika Pumzika kwa amani Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli tutakukumbuka daima.

Katika kipindi cha uongozi wake hayati Rais John Magufuli alihudhuria michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara, mchezo wa kwanza uliokuwa Simba dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa tarehe 19 Mei, 2018 ambapo Simba alikabidhiwa ubingwa wa Ligi Kuu.

Na mchezo mwengine ulikuwa kati ya Simba na Yanga uliopigwa tarehe 8 Machi, 2021 ambao ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!