May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Klabu za Ligi kuu za mpongeza Rais Samia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Saluhu akihutubia Taifa mara baada ya kuapishwa

Spread the love

 

MARA baada ya kuapishwa kuwa Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, klabu mbalimbali za Ligi Kuu soka Tanzania Bara zimetuma salamu zao za pongezi mara baada ya tukio hilo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Rais Samia ameapishwa hii leo tarehe 19 Machi, 2021 Ikulu Dar es Salaam kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi 2021 kwenye hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam.

Klabu hizo zilituma salamu hizo za pongezi kupitia kurasa zao tofauti zilizopo kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram, Twitter na Facebook.

Kwa upande wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, klabu ya Simba wao waliandika kuwa uongozi, wachezaji pamoja na benchi la ufundi la klabu ya Simba, unatoa pongezi nyingi kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mabingwa wa kihistoria klabu ya Yanga wao waliandika kuwa “Kwa niaba ya wapenzi, wanachama na mashabiki wa klabu ya Yanga tunamtakia kila la kheri na mafanikio katika kuongoza nchi yetu”

Nao klabu ya Dodoma Jiji ambao wanatoka makao makuu ya nchi kupitia ukurasa wao wa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram nao walituma pongezi zao.

error: Content is protected !!