August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

KKKT Mashariki na Pwani kwafukuta

Askofu Dk Malasusa

Spread the love

SAKATA la vyeti feki, limetinga ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, anaandika Mwandishi Wetu.

Naibu Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Mchungaji Ernest Kadiva, alitangazia watumishi wote kwenda kuondoa nakala za vyeti vyao kwenye mafaili kwa kuwa “ni feki.”

Akizungumza katika mkutano wa pamoja na watumishi wote, Kurasini jijini Dar es Salaam, Mchungaji Kadiva amesema, “uhakiki wa vyeti umelenga kulisafisha kanisa.”

Taarifa zinasema, tangazo hilo lililotolewa na naibu katibu mkuu wa dayosisi hiyo, liliwaudhi baadhi ya watumishi kwa madai kuwa limewalenga baadhi ya watu.

Hata hivyo, mtoa taarifa wa gazeti hili amesema, suala la vyeti feki laweza kumkumba hadi mkuu wa dayosisi hiyo, Askofu Dk. Alex Malasusa.

“Hata mkuu wetu hawezi kubaki salama katika sakata hili. Naye

ni mmoja wa watuhumiwa wakuu katika sakata hili la vyeti feki. Anatuhumiwa hata kujipachika shahada ambazo hakuwahi kuzisomea,” anaeleza.

Amesema, “sisi huyu jamaa tunamjua tangu utoto wake. Alimaliza kidato cha nne na kushindwa mtihani, lakini hivi sasa anadai ana shahada ya pili (masters) kutoka chuo kikuu kimoja nchini Kenya.”

Alipoulizwa katibu mkuu wa Askofu Malasusa, Godfrey Nkini aligoma kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa ni mgeni katika nafasi hiyo na “silijui undani wake.”

Mtoa habari amesema, “huko nyuma mkuu wetu alitaka kutumia kigezo cha vyeti feki kuwafukuza wabaya wake, lakini sasa naye anatuhumiwa.”

“Kuna wachungaji walisimamishwa, wengine walizuiwa kuendelea na masomo na hata wengine kuacha kazi kwa kudaiwa walitumia vyeti feki kuingia katika uchungaji,” ameeleza mtoa taarifa.

Baadhi ya wachungaji waliosimamishwa na baadaye kurejeshwa kazini ni Paulo Lusambi, Leona Kimaro, Nkya, Mchome, Mbaga na Mgaya.

Aidha, imeelezwa kuwa yuko mwanamke mmoja aliyeruhusiwa na Askofu kwenda masomoni akiwa na cheti feki na kumaliza chuo, lakini Askofu aligoma kumbariki kwa kudai ana cheti feki.

Mtoa habari anasema, sababu ya cheti ilitumika kufunika sababu halisi ya Askofu kukataa kumbariki mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa.

Mwinjilisti mmoja kutoka Jimbo la Kusini ndani ya dayosisi hiyo alisimama na kufoka kuwa “wako wachungaji wengi waliobarikiwa na wana vyeti feki.”

Akahoji, “kwa nini sisi wainjilisti na parish workers tunaonewa na kuachwa wengine.”

Mwaka mmoja uliyopita, Askofu Malasusa aliitisha vyeti vya wachungaji kadhaa kwa madai kuwa vilikuwa vimeghushiwa.

Baada ya mjadala, baadhi waliomba radhi na kusamehewa lakini ilibainika wakati huo kuwa hata yeye alikuwa anatumia cheti bandia cha kidato cha nne na pia kujaza katika wasifu wake (CV) yake habari za uwongo kuwa alisoma Chuo Kikuu Katoliki nchini Kenya.

Hivi karibuni Askofu Malasusa amepeleka kundi la watu 40 kusomea uchungaji huko Mwika-Moshi, lakini Naibu Katibu Mkuu Mchg Bon Kombo alipolekeka vyeti baraza la mitihani, aliambiwa asilimia 80 ya vyeti hivyo ni feki na walitakiwa kurudishwa.

“Askofu Malasusa alimua wabaki huko na wasome programu maalum na kuwa atawabariki wakimaliza.”

Wachungunzi wa mambo katika dayosisi hiyo wanadai Askofu Malasusa baada ya kukabiliwa na tuhuma mbaya za maadili anaandaa jeshi la kumlinda kwa kupeleka watu wenye vyeti feki katika kazi ya uchungaji.

Taarifa zinasema, tuhuma pia kuwa ameanzisha vita na watu wanaotoka Kaskazini huku akiingiza watu wengi kutoka Mbeya katika mkakati wa kujilinda.

 

error: Content is protected !!