August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kizza Besigye aachiliwa kwa dhamana Uganda

Kizza Besigye

Spread the love

 

ALIYEKUWA mgombea urais nchini Uganda, Dk. Kizza Besigye na mshtakiwa mwenzake Samuel Lubega Mukaaku wamepewa dhamana ya pesa taslimu ya Sh2.5 milioni kila mmoja. Anaripoti Mwandishi Wetu kwa msaada wa mitandao … (endelea)

Vilevile wawili hao wameamriwa kutotoa maoni yoyote hadharani kuhusu kesi hiyo hadi itakapokamilika kusikilizwa.

Wanaharakati hao wawili wa kisiasa ambao wamekuwa kizuizini tangu Juni 15 mwaka jana walipokamatwa katikati mwa jiji la Kampala walifikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mahakama ya Barabara ya Buganda iliyoongozwa na Kaimu Jaji wa Mahakama Kuu Douglas Singiza.

Hatua hiyo inajiri siku moja tu baada ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Kampala, Tadeo Asiimwe kukataa ombi lao la dhamana.

Daktari Kiiza Besigye amekuwa gerezani Luzira kwa muda wa majuma mawili kwa mashitaka ya uchochezi wa ghasia miongoni mwa wananchi baada ya kufanya maandamano ya kupinga kupanda kwa bei za bidhaa nchini Uganda.

Watuhumiwa hao walikana mashitaka yote.

Bei ya Petrol na Dizel nchini Uganda ni shilingi 6200 kwa lita moja sawa na dola za Marekani 1.8, kutoka bei ya 4,500 mwaka jana.

Rais Museveni katika hotuba yake kwa taifa alifahamisha tatizo la mfumuko wa beini la dunia nzima, hivyo kupunguza kodi kwenye mafuta itaathiri mipango ya maendeleo ya taifa kamavile miundo mbinu.

Bei ya mafuta imesababisha kupanda kwa kila bidhaa nchini Uganda.

error: Content is protected !!