BAJETI ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeibua kizaazaa bungeni baada ya wabunge waliokuwa wakichangia kufanya matukio yasiyo ya kawaida kuonesha kusikitishwa na utekelezaji wa miradi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Leo Jumatatu tarehe 23 Mei, 2022 Mbunge wa Ukonga, Jerry Slaa, ambaye alikuwa wa kwanza kuchangia mara baada ya bajeti hiyo kuwasilishwa na Waziri Profesa Makame Mbarawa.
Akichangia hotuba hiyo Slaa amejikuta akilia machozi kwa kile alichodai uchaguzi umekaribia huku utekelezaji wa miradi ya barabara ukiendelea kusuasua.
Mbunge huyo ambaye amewahi kuwa Meya wa Manispaa ya Ilala amesema kumekuwepo na wakandarasi ambao hawazingatii ubora wa barabara ikiwemo ile ya Mwendokasi ya Mbagala.
Amesema tatizo hilo linatokana na makandarasi mmoja kupewa kazi zaidi ya nne aklitpolea mfano wa kampuni ya Sino-Hydro.
Amesema kampuni hiyo imesema mkandarasi huyo ana kazi sita ikiwemo ya ujenzi wa barabaraya mwendokasi kutoka Kariakoo-Mbagala.
“Mkandarasi huyo ambaye kilomita 25 zimekutwa na ufa, mkandrasi huyo amabye halipi wafanyakazi, asiyelipa wazabuni ameenda kuongezewa kazi nyingine,” amesema.
Ameongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan alishaonya kuhusu mkandarasi kupewa kazi nyingi lakini bado Sino Hydro ameendelea kupewa kazi nyingi.
Amesema kero hiyo inapelkwa tena kwa wananchi wa Gongo la Mboto kwa mkandarasi huyo kuendelewa kupewa tenda za ujenzi licha ya kutekeleza chini ya kiwango.
“Hatuwezi kuacha watu hawa wakaendelea kufanya kazi hiyo. Kuna jambo nilisema hapa kuhusu single source sio mbaya tatizo ni uadilifu wa wale wanaosimamia kazi hizi,” amesema.
Mbunge huyo amnae kitaaluma ni mwanasheria amesema awamu ya kwanz aya mradi kutoka Kimara hadi Kivukoni ulijengwa na Kampuni ya Strabag “leo miaka saba hakuna shimo moa lililotopkea hivi wangempa phase iii single source Strabag kuna mtu angelalamika?”
Ametolea mfano mwingine wa mradi wa maji Arusha wenye awamu 13 ambapo alisema awamu 12 zimekamilika lakini awamu moja aliyopewa Sino-Hydro haijakamilika hadi sasa.
Mbali na Slaa Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay yeye amelazimika kupanda juu ya meza bungeni na kubinuka sarakasi kwa kile alichodai ni kuonesha kukasirika kwa jimbo lake kutojengwa barabara ya lami licha ya Serikali kuahidi katika kila bajeti.
Hii ni mara ya pili kwa mbunge huyo kutaka kupiga sarakasi baada ya Mei 17, 2021 akichangia bajeti ya Uchukuzi kutishia kufanya hivyo kabla ya Naibu Spika wakati huo Tulia Akson kumtaka asifanye hivyo.
Awamu hii ameamua kupiga sarakasi na kuahidi kushika shilingi ya Wizara hiyo endapo hatopewa majibu ya kuhusu ujenzi wa barabara ya lami jimbo la Mbulu Vijijini.
“Waananchi wa Mbulu hawajui barabara ya lami kabisa lakini hapa kuna barabara zingine zinakwenda kukarabatiwa ina maana hawa wameshakaa na barabara kwa muda mrefu na sasa zinaenda kuboreshwa,” amesema Massay.
“Nimeonesha kuwa nimekasirika Mh. Waziri na nitakwenda kushika shilingi niende nayo kwa watu wa Mbulu,” amesema.
Leave a comment