November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kiza kinene kimeikumba nchi

Spread the love

GIZA limetanda katika maeneo yote yanayopata umeme kupitia gredi ya taifa jijini Dar es Salaam na mikoa mingine nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Umeme la Taifa (Tanessco), usiku wa manane wa leo Jumamosi inasema, “shirika linawaomba radhi wateja wake wa mikoa iliyounganishwa na gridi ya taifa kwa katizo la umeme lililotokea leo Disemba 29, 2018 majira ya saa tisa usiku.”

Tanesco inarejea sababu zilezile za kukatika umeme, kuwa “ni hitilafu iliyotokea katika mfumo wetu wa gridi.”

Inasema, “wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na jitihada za kuhakikisha umeme unarejea kwa haraka katika maeneo yote.

“Tutaendelea kutoa taarifa kadiri kazi inavyoendelea.

“Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.”

Hata hivyo, taarifa hiyo iliyotolewa na Idara ya Uhusiano ya shirika hilo, haikuleza umeme huo unatarajiwa kurejea baada ya muda gani.

error: Content is protected !!