SERIKALI nchini Tanzania, inatarajia kuanza ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwada, mkoani Manyara. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).
Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu tarehe 3 Mei 2021, na Mwita Waitara, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu.
Waitara alikuwa akijibu swali la Regina Qwaray, Mbunge wa Viti Maalum mkoani Manyara (CCM), aliyetaka kujua lini serikali itaweka mpango wa ujenzi wa kiwanja hicho mkoani Manyara.
Waitara amesema, serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), na kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, wameainisha eneo la Mwada katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja hicho.
Leave a comment