Saturday , 3 June 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini China chaongezeka
Kimataifa

Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini China chaongezeka

Xi Jinping, Rais wa China
Spread the love

 

WAKATI kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana nchini China kinazidi kuongezeka ikiwa wengine mamilioni wakikaribia kuhitimu vyuo vikuu. Imeripotiwa na ANI News … (endelea).

Wizara ya Elimu ya China inaeleza kuwa wanafunzi milioni 11.6 wa Vyuo Vikuu wanatarajiwa kuhitimu Juni mwaka huu.

The Straits Times iliripoti kuwa juma lililopita serikali iliweka wazi kuwa asilimia 20.4 ya watu wenye umri wa miaka 16 hadi 24 wanaotafuta kazi walikosa nafasi.

Inaelezwa kuwa kwa sasa China imefika kiwango cha ukosefu wa ajira kwa kika wahitimu watano mmoja anakosa ajira na kwamba hicho ni kiwango cha juu.

China hawana kazi, kiwango cha tangu China ilipoanza kutangaza takwimu kama hizo mwaka 2018.

Mkuu wa usimamizi wa fedha katika chuo kimoja huko Chengdu, alisema maombi ya wahitimu 100 wa chuo chao yamekubaliwa maombi matano.

Shu Xiang kijana wa miaka 21, anayehangaika kutafuta kazi tangu ahitimu elimu yake ya juu anasema kuwa ukosefu wa ajira umeanza kukomaa.

“Sina uhakika wa kupata kazi,” alisema Shu.

Mwezi Machi Mwaka huu, orodha za nafasi za kazi katika utalii na usafirishaji wa abiria na mizigo zilikua kwa kasi zaidi, kwa mujibu wa tovuti ya Zhilian.

Mtafiti katika Taasisi ya Fedha na Sheria ya Shanghai, Dk. Nie Riming, alisema vijana wenye shahada za elimu ya juu wanatafuta kazi za teknolojia, elimu na udaktari.

“Lakini viwanda hivi ndivyo hasa ambavyo vimekuwa vikikua polepole nchini China katika miaka kadhaa iliyopita,” alisema Dk Nie.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Kauli ya Rais wa China kuhusu ajira yawakatisha tamaa vijana

Spread the love  KAULI ya hivi karibuni ya Rais wa China, Xi...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Jeshi la Sudan lasitisha mazungumzo na wanamgambo wa RSF

Spread the love  JESHI rasmi la serikali ya Sudan, limesitisha ushiriki wake...

Kimataifa

Wakimbizi laki mbili wa Kongo, Burundi kuhemea chakula

Spread the love  SHIRIKA la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP), limetangaza...

Kimataifa

Mkutano wa Quad Hiroshima waibuka na kutafuta amani na ustawi wa Indo-Pacific

Spread the love  JITIHADA za mazungumzo ya Pande Nne (Quad), hazikuthaminiwa na...

error: Content is protected !!