June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kiwanga ataka Moro igawanywe

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeria (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chadema wa Morogoro, Suzan Kiwanga

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum, Suzan Kiwanga (Chadema), ameitaka Serikali kuingilia kati mgogoro ambao unaonekana kukua kati ya majimbo ya Ulanga Mashariki na Ulanga Magharibi. Anaandika Dany Tibason …(endelea).

Kiwanga alitoa pendekezo hilo bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza akitaka kujua ni lini mgogoro wa ugawaji majimbo katika mkoa wa Morogoro utatatuliwa.

Awali katika swali lale la msingi, Kiwanga alitaka kujua ni lini serikali itatangaza kuugawa mkoa wa Morogoro kwa kuzingatia maombi na mapendekezo ya RCC ya tangu mwaka 2013, na kuhoji ni lini serikali itaridhia mapendekezo ya kugawa jimbo la Kilombero kwa majimbo mawili ili kusogeza huduma kwa wananchi.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kasim Majaliwa amesema kuwa suala ya kugawa mkoa wa Morogoro liliibiliwa katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichokutana 10 Januari mwaka jana.

“Katika kikao hicho ilipendekezwa uanzishwe mkoa mpya wa Kirombelo na kuanza mchakato wa kitaalam ufanyike ikiwa ni pamoja kuwasilisha mapendekezo hayo Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi).

“Hadi sasa pendekezo hilo halijapitishwa katika vikao vya kisheria ili kuwezesha serikali kufanya maamuzi kwa kuzingatia vigezo na maoni ya vikao vya kisheria,” alieleza Majaliwa.

Kuhusu mgogoro ambao aliutaja Kiwanga katika majimbo ya Ulanga Mashariki na Magharibi, amesema kuwa serikali itahakikisha inaingilia kati ili kuutatua.

error: Content is protected !!