January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kiwanga ahoji Kilombero kutelekezwa

Kivuko cha Kilombero

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalumu, Suzan Kiwanga (Chadema), ameibana Serikali itoe majibu ya kina ni kwa nini imeitelekeza Wilaya ya Kilombero katika ujenzi wa vituo vya Polisi. Anaandika Dany Tibason …(endelea).

Kiwanga alitoa kauli hiyo katika swali la nyongeza, akisema kuwa polisi katika wilaya hiyo inatumia majengo mengi ya taasisi za Umma tofauti na maeneo mengine nchini ambako wamejengewa majengo yao.

“Ukiacha kituo cha Mlimba ambako wanatumia majengo ya Tazara, lakini bado pia kituo cha wilayani Kilombero nacho Polisi inatumia majengo ya Maliasili, hivi wilaya hiyo tuliwakosea nini Serikali? Amehoji.

Awali katika swali la msingi, mbunge huyo alitaka kujua ni lini serikali itajenga kituo cha Polisi cha Mlimba ili kuondokana na adha ya majengo ya Tazara ambayo bado hayakidhi mahitaji ya kituo hicho.

Naibu Waziri wa Jamii, Jinsi na Watoto, Dk. Pindi Chana, alikiri kuwepo na tatizo hilo katika kituo cha Tarafa ya Mlimba ambacho kinahudumia kata saba.

Amezitaja kata zinazohudumiwa na kituo hicho kuwa ni Kamwene, Utengule, Kalengakero, Chisano, Uchindile na Masagati ambapo wanatumia majengo ya Tazara, ambayo hayakidhi huduma za ulinzi kwa eneo hilo lenye wakazi 40,202.

Dk. Chana amesema serikali inatambua umuhimu wa kujenga vituo vya Polisi kwa nchi nzima ambako maeneo mbalimbali kunaonekana kuwa na upungufu.

“Katika bajeti ya mwaka huu, kiasi cha Sh. 8 bilioni zimetengwa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya, hivyo wilaya ya Kilombero itapewa upendeleo wa pekee katika bajeti ya mwaka huu,” amesema Chana.

error: Content is protected !!