Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kiwanda Kilombero champa mashaka Waziri Mkuu Majaliwa
Habari za Siasa

Kiwanda Kilombero champa mashaka Waziri Mkuu Majaliwa

Spread the love

KASSIMU Majaliwa, Waziri Mkuu amehoji sababu za Kiwanda cha Sukari cha Kilombero chenye uzalishaji mkubwa kuliko viwanda vingine vya sukari nchini, kutoa gawio dogo serikalini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda hicho tarehe 17 Septemba 2019, Majaliwa amesema hajaridhishwa na gawio la kiasi cha Sh. 800 milioni kinachotolewa na Kilombero huku Kiwanda cha Sukari cha Moshi TPC, chenye uzalishaji mdogo kikitoa Sh. 15 bilioni kwa mwaka.

Majaliwa ameagiza uongozi wa kiwnada hicho, kufanya mabadiliko ya kiasi cha gawio kinachopelekwa serikalini ili uwekezaji huo uwe na tija kwa pande zote mbili, kwa mwekezaji na serikali.

“Baada ya kuwa tumeweka utaratibu mzuri, tumeona kila kampuni ambayo na sisi tuna hisa tunaanza kupata gawio, nyie bado kiwango hakitoshi wenzenu TPC wametoa Bil. 15, na nyie ni moja, milioni 800 nilisema bil 1 kumbe nimekusogeza sogeza hazitoshi,” amesema Majaliwa na kuongeza;

“Mmemiliki kwa asilimia 75  milioni 800 ni ndogo na hiki ndio kiwanda kikubwa kuliko vyote nchini na uzalishaji wake ni mkubwa kwa hiyo tunahitaji kuona mabadiliko kwenye gawio. Ili na sisi tuone tuna muwekezaji tunayejivunia, na uwekezaji huu uendelee kuwa na tija.”

Aidha, Majaliwa ameagiza viwanda vya sukari nchini kuzalisha sukari ya kutosha ili kukidhi mahitaji, kwa kuwa nchi ina uhitaji mkubwa wa bidhaa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!